Timu yatua salama Morocco

Kikosi chetu kimewasili salama nchini Morocco tayari kwa mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Mohamed wa V.

Kikosi kimeondoka jana usiku ambapo kimepitia Dubai na baadaye Tunisia kabla ya kufika Morocco.

Baada ya kufika kesho kikosi kitafanya mazoezi ya kwanza hapa Morocco kujiweka sawa kabla ya mtanange huo ambao tunafahamu utakuwa mgumu.

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri hakuna aliyepata madhara kutokana uchovu wa safari ndefu.

Tutaingia katika mchezo wa Ijumaa ambao utapigwa saa tatu usiku kwa saa za Tanzania tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja tulilopata kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi iliyopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER