Timu yatua salama Kilimanjaro

Kikosi chetu kimewasili salama mkoani Kilimanjaro tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Ushirika.

Baada ya kuwasili wachezaji watapumzika usiku wa leo na kesho watafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa kabla ya mchezo huo.

Ingawa hatukupata ushindi kwenye mchezo uliopita lakini morali za wachezaji iko juu kuhakikisha wanapambana kuwapa furaha Wanasimba.

Tunafahamu umuhimu wa pointi tatu katika mchezo wa Jumapili na kila mchezaji atakayepewa nafasi atakuwa tayari kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER