Timu yatua salama Dar

Kikosi chetu kimerejea salama jijini Dar es Salaam kutoka nchini Angola baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto uliofanyika jana jioni.

Baada ya kikosi kurejea wachezaji wamepewa mapumziko ya kwenda kukutana na familia zao kabla ya kuanza maandalizi mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Kesho kikosi kitaanza mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena na Jumatano kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mtanange huo muhimu ambao utatupa kibali cha kuingia hatua ya makundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER