Timu yatembelea Ubalozi nchini Uturuki

Kikosi chetu leo kimetembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki na kuzungumza mambo mbalimbali na mwenyeji wetu, Balozi Luteni Jenerali, Yakubu Hassan Mohamed.

Luteni Jenerali, Yakubu ametutakia maandalizi mema kuelekea mashindano yaliyo mbele yetu huku akiwakumbusha wachezaji kuhakikisha wanapambana uwanjani kusaidia timu kupata ushindi.

“Nimefurahi sana kukutana nanyi hapa, nawakaribisha sana Uturuki jisikieni mpo nyumbani, sisi tutahakikisha mnapata kila kitu ambacho mnastahili.

“Binafsi niwatakie maandalizi mema kuelekea msimu mpya wa mashindano, kikubwa nasisitiza kwa wachezaji mjitume uwanjani kuipa timu ushindi na kuwapa furaha mashabiki,” Balozi Yakubu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER