Timu yarejea, Zimbwe Jr atoa neno

Nahodha wa timu Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kikosi chetu kipo tayari kupambana hadi mwisho katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli utakaopigwa siku ya Jumapili.

Zimbwe Jr amesema tunajua utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Al Ahli Tripoli lakini tupo kwenye ardhi ya nyumbani tukiwa tunajua nyuma kuna mashabiki wetu.

Zimbwe amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu kwakuwa wana mchango mkubwa kutimiza malengo ya kuisaidia timu kufika hatua ya makundi.

“Tumerudi salama nyumbani, tukiwa na nguvu na ari ya kupambana kuhakikisha tunaibuka na ushindi na kutinga hatua ya makundi ya michuano hii.”

“Al Ahli Tripoli ni timu bora na walitupa upinzani mkubwa pia walipata nguvu kubwa kutoka kwa mashabiki wao, nasi tunaamini Jumapili tutakuwa na mashabiki wetu hivyo tupo kwenye nafasi yakufanya vizuri,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER