Timu yarejea salama Dar, Wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi chetu kimerejea salama jijini Dar es Salaam kutoka mkoani Kilimanjaro baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania uliopigwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Baada ya kuwasili wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja na kesho mazoezi ya kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union yataanza.

Desemba 3, kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga kuikabili Coastal.

Tunajua mchezo dhidi ya Coastal utakuwa mgumu na ndiyo maana maandalizi yataanza mapema kesho ili kuhakikisha tunaenda kupambana na kupata alama tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER