Timu yarejea salama Dar es Salaam

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam usiku huu kutoka Tanga baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union.

Kikosi kimeondoka Tanga mchana baada ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuwaweka wachezaji sawa kabla ya kuanza safari.

Baada ya kufika wachezaji wameruhusiwa kwenda kupumzika na kesho mchana kikosi kitaingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Jumanne saa moja usiku Uwanja wa Azam Complex.

Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho jioni katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena tayari kwa kuwavaa Singida.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER