Timu yarejea mazoezini kujiandaa na Power Dynamos

Kikosi chetu kimeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex, Oktoba Mosi saa 10 jioni.

Wachezaji walipewa mapumziko ya siku mbili baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union tulioibuka na ushindi wa mabao 3-0 tuliocheza Alhamisi na leo tumeanza rasmi mawindo ya Power Dynamos.

Wachezaji wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Mo Simba Arena na wamejitahidi kufuata maelekezo kwa umakini waliyokuwa wanapewa na makocha.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi siku ya Jumapili.

Programu ya mazoezi itaendelea kesho chini ya kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER