Kikosi chetu leo kimerejea mazoezini kuanza maandalizi ya michuano ya Mapinduzi ambayo yanaanza Disemba 28 mpaka Januari 13 Visiwani Zanzibar.
Baada ya mchezo dhidi ya KMC wachezaji walipewa mapumziko ya siku tatu kwenda kusherehekea sikukuu ya Krismasi na leo wamerejea mazoezini.
Kikosi kitaendelea na mazoezi chini ya Kocha Benchikha na wasaidizi wake hadi kitakapoanza safari ya kuelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo.
Tumepangwa kundi B pamoja na timu za JKU, APR na Singida Fountain Gate ambapo mchezo wetu wa kwanza utakuwa dhidi ya JKU Januari Mosi katika Uwanja wa Amaan saa 2:15 usiku.