Timu yarejea mazoezini, Kuifuata Prisons Jioni

Kikosi kimefanya mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Alhamisi saa 10 jioni katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake baada ya mapumziko ya siku ya siku moja.

Baada ya mazoezi hayo wachezaji watapumzika kwa saa chache kabla ya leo jioni kuaanza safari ya kuelekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo.

Kesho timu itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani Alhamisi.

Tunatarajia kusafiri na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo kwakuwa lengo letu ni kuhakikisha tunarudi na alama tatu ugenini.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER