Timu yarejea mazoezini

Baada ya mapumziko ya siku mbili wachezaji wamerejea mazoezini kujiandaa na mechi mbili zilizozalia za Ligi Kuu ya NBC.

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena chini ya Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ pamoja na wasaidizi wake.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri morali ikiwa juu kuhakikisha tunapata pointi tatu kwenye michezo hiyo.

Mchezo wetu inayofuata utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigiwa Juni 6, wakati wa mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Coastal Union Juni 9 na zote tutakuwa nyumbani.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER