Timu yarejea mazoezini

Baada ya mapumziko ya siku nne waliopewa wachezaji leo asubuhi kikosi chetu kimerejea mazoezini kujiandaa na mechi mbili za Ligi Kuu ya NBC zilizosalia.

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena chini ya kocha mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ na wasaidizi wake.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kujiandaa na mechi zilizobaki.

Mchezo wetu unaofuata utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulisogezwa mbele lakini bado haujapangiwa tarehe ya kuchezwa.

Tunaamini mchezo huo utapigwa wiki ijayo ndio maana kikosi kimerejea mazoezini kujiandaa ili tarehe itakapotangazwa tuwe tayari.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER