Kikosi chetu kimerejea jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma baada ya jana kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Jamhuri.
Kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuondoa uchovu wa mechi.
Kesho Kikosi kitaanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Oktoba 4 katika Uwanja wa KMC Complex saa 10:15 jioni.