Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam leo kutoka mkoani Mbeya huku wachezaji wakipewa mapumziko ya siku moja.
Kesho kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wetu unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumamosi Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Matokeo ya jana dhidi ya Mbeya City yametufanya kuchukua tahadhari katika kila mchezo uliopo mbele yetu hivyo mashabiki wetu watarajie mabadiliko yatakayoambatana na ushindi.
One Response