Timu yarejea Dar, Wachezaji wapewa mapumziko

 

Kikosi kimerejea mchana jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma baada ya ushindi wa bao moja tuliopata jana dhidi ya Dodoma Jiji.

Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi, Benjamin Mkapa.

Mazoezi hayo yatafanyika saa 10 jioni katika Uwanja wa Mo Simba Arena ambapo wachezaji wote wanatarajiwa kuhudhuria.

Lengo letu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa michuano hii na tunapaswa kushinda kila mchezo tukianza na Coastal, Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER