Timu yarejea Dar, Wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam kutoka Mwanza baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC katika Uwanja wa CCM Kirumba jana.

Baada ya kuwasili wachezaji wamepewa mapumziko ya kwenda kukutana na familia zao na kesho tutaanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Ijumaa, Desemba 30.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema lengo letu lilikuwa kuchukua pointi zote tisa za Kanda ya Ziwa kwenye mechi tatu lakini tumefanikiwa kupata saba.

“Kikosi kimerejea salama Dar es Salaam na wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja na kesho tutarudi mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons,” amesema Rweyemamu.

Katika mechi tatu za Kanda ya Ziwa tumeshinda mbili dhidi ya Geita (5-0), KMC (3-1) na sare ya bao moja na Kagera Sugar.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER