Timu yapaa yaifuata Al Ahly Misri

Kikosi chetu kimeondoka alfajiri kuelekea Cairo, Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa saa tano usiku.

Kikosi chetu kinatarajia kufika jijini Cairo saa tano asubuhi ambapo wachezaji watapumzika kwa saa chache kabla ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili.

Alhamisi timu itafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Cairo saa tano usiku muda ambao mchezo wetu utapigwa siku ya Ijumaa kama kanuni za CAF zinavyoelekeza.

Kikosi kimeondoka na jumla ya wachezaji 23.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER