Timu yaingia kambini rasmi kujiandaa na Raja

Kikosi chetu kimeingia kambini rasmi leo kujiandaa na mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baada ya kikosi kuwasili jana alfajiri wachezaji walipewa mapumziko kutokana na uchovu wa safari ndefu na leo wachezaji wamefanya mazoezi na kuingia kambini moja kwa moja.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Mo Arena chini ya kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anaonekana kuhitaji kuaminiwa ili kupata nafasi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Raja.

Uongozi unaendelea kusisitiza mashabiki kukata tiketi mapema ili kuepeuka usumbufu tayari kampeni ya hamasa imezinduliwa leo Tegeta na kila sehemu itakapopita zitaendelea kuuzwa hadi siku ya mchezo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER