Timu yaingia Kambini kujiandaa na Wydad Jumamosi

Kikosi chetu kimeingia kambini leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca kutoka Morocco utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Mchezo wetu utapigwa saa 10 badala ya saa moja usiku kama ilivyozoeleka katika hatua ya makundi kwakuwa itakuwa ni sikukuu ya Eid El Fitr.

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga juzi Jumamosi wachezaji walipewa mapumziko kabla ya leo kuingia kambini moja kwa moja.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema wachezaji wawili Sadio Kanoute ambaye hakuonekana katika mechi kadhaa zilizopita kutokana na majeruhi pamoja na Aishi Manula nao watafanyiwa vipimo.

“Sadio alipata maumivu ya nyonga na leo atafanyiwa vipimo kama itaonekana yupo fiti ataanza mazoezi pamoja na wenzake kama ilivyo kwa mlinda mlango Manula kwahiyo itategemea majibu ya vipimo ili kujua kama wawili hawa watakuwa sehemu ya kikosi,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER