Timu yaingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons

Kikosi chetu kimeanza mazoezi pamoja na kuingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Jumatano katika Uwanja Jamhuri mkoani Morogoro.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema sasa ni rasmi tutatumia Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro kwa mechi zetu za nyumbani na mechi dhidi ya Prisons itakuwa ya kwanza.

Ahmed amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo na lengo letu litakuwa kupata pointi tatu muhimu.

Ahmed amewaomba mashabiki wetu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya Jumatano kwa ajili ya kuispoti timu.

“Tumemaliza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika sasa tunarejea kwenye Ligi Kuu na Jumatano tutashuka dimbani kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao utapigwa katika Uwanja wa Jamhuri.”

“Kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani, tunahitaji furaha tuliyopata Jumamosi tuendelee nayo,” amesema Ahmed.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER