Timu yafika salama Uturuki

Baada ya kuanza safari kutoka Dar es Salaam jana saa 9:55 Alasiri kikosi chetu kimewasili salama Istanbul, Uturuki leo saa 7:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki .

Baada ya kuwasili msafara ulipokelewa na Msaidizi wa Balozi nchini Uturuki, Abdullah Alfan ambaye alikuwa mwenyeji wetu kwenye mambo yote ya msingi hadi masuala ya uwanja wa ndege yanamalizika.

Taratibu za kutoka Uwanja wa Ndege zilipokamilika msafara ulichukuliwa na basi maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kwenda kwenye mji wa Ankara ambapo ndipo tutakapoweka kambi yetu kwa ajili ya maandalizi ya msimu (Pre-season).

Mratibu wa timu, Abbasi Ally ambaye alitangulia kwenda kuweka mambo sawa amesema kila kitu kimekwenda kama kilivyopangwa na taratibu zote zinaendelea vizuri.

“Jambo zuri ni kuona kila mchezaji ana morali ya hali ya juu, naamini kila kitu kitaenda sawa na ratiba yetu itakuwa kama tulivyoipanga,”amesema Abbas.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER