Timu yafanya mazoezi ya utimamu kabla kuanza safari kuelekea Tanga

Kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili saa tatu asubuhi kabla ya kuanza safari ya kuelekea jijini Tanga tayari kwa mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi.

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Prisons wachezaji wamefanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika Uwanja wa Highland na mchana kitaelekea Tanga.

Pamoja na kupata matokeo tusiyo yatarajia jana wachezaji wapo kwenye hali nzuri na hawakuvunjika moyo, wapo tayari kupigania timu.

Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho jioni katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga tayari kwa mchezo wa Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER