Timu yafanya mazoezi ya mwisho

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny tayari kwa kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa kesho saa nne usiku.

Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo na wapo tayari kwa mchezo.

Kufanya mazoezi katika Uwanja huu ni sehemu ya matakwa ya kikanuni ambayo kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambalo linataka timu mgeni kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa mchezo siku moja kabla.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER