Timu yafanya mazoezi ya mwisho Zanzibar

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya KVZ utakaopigwa kesho saa 2:30 Usiku.

Wachezaji wote 26 ambao tumesafiri nao kuja Zanzibar wameshiriki mazoezi hayo wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho.

Kikosi kiliwasili hapa Zanzibar mchana na wachezaji walipata saa chache za kupumzika kabla ya kufanya mazoezi.

Tumekuja Zanzibar kwa lengo la kupambana na kuchukua ubingwa wa michuano hii.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER