Timu yafanya mazoezi ya mwisho TTC Mtwara

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika Uwanja wa TTC Mtwara tayari kwa mchezo wa kesho wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC.

Mchezo wetu wa kesho utaanza saa 9:30 Alasiri katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona ambapo tunaamini utakuwa mgumu.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri, hakuna yoyote ambaye tutamkosa kutokana na kupata maumivu.

Kocha mkuu Robertinho pamoja na wasaidizi wake watakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi sababu wachezaji wote wapo tayari.

Baada ya kukamilika kwa mazoezi tulienda kutembelea Uwanja wa Nangwanda Sijaona (feel the pitch) ambao tutautumia kesho kama inavyopaswa kwa mujibu wa kanuni kwakuwa hatujafanya mazoezi ya mwisho hapo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER