Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena kujiandaa na Ihefu

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC utakaopigiwa saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa.

Baada ya kikosi kurejea jijini Dar es Salaam jana kutoka mkoani Singida kiliingia kambini moja kwa moja tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa kesho.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi isipokuwa Peter Banda aliyepata majeraha kwenye mchezo uliopita na wale majeruhi wa muda mrefu Jimmyson Mwanuke na Israel Patrick.

Ingawa Ihefu ipo mwisho kwenye msimamo lakini hatuwadharau na tutaingia kwa tahadhari zote kwa kuwa tunahitaji kupata alama tatu nyumbani.

Morali ya wachezaji ipo juu na wamefanya jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi kwenye mchezo wa kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER