Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kuanza safari mchana kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Jumamosi.

Mazoezi hayo yamesimamiwa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake ambapo wachezaji wote wameshiriki.

Baada ya mazoezi wachezaji watapumzika kwa saa chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea Morocco ambapo watapitia Doha Qatar na kubadili Ndege hadi Casablanca na baadae kubadili tena hadi Marrakech ambapo mechi itafanyika.

Kikosi kinatarajia kuondoka na nyota 23 ambao tunaamini wataweza kutupatia matokeo chanya katika mchezo huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER