Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

Mchezo wa kesho utapigwa saa 10 jioni Azam Complex Chamazi kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kuendelea na ukarabati.

Wachezaji wote ukiacha wale amjeruhi watatu mlinda mlango Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Power Dynamos lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana tunashinda na kufuzu hatua ya makundi.

Malengo yetu ni kufika nusu fainali ya michuano hii kwahiyo ili kufanikisha jambo hili tunapaswa kufika hatua ya makundi kwa kuitoa Power Dynamos kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER