Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Kikosi kinaondoka nchini saa 9 Alasiri kuelekea Morocco tayari kwa mchezo huo ambao utakuwa wa mwisho wa hatua ya makundi.

Kikosi kitaondoka na wachezaji 13 pamoja na benchi la ufundi huku wale ambao wapo kwenye majukumu ya timu za taifa wataungana moja kwa moja na timu ikiwa Morocco.

Mchezo wetu utapigwa Machi 31 saa nne usiku kwa muda wa Morocco ambapo huku kwetu itakuwa Aprili Mosi saa saba usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER