Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa kesho kwenye dimba la Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Wachezaji wawili Shomari Kapombe na Jimmyson Mwanuke ndio pekee ambao hawakushiriki mazoezi hayo kutokana na kuwa majeruhi lakini wengine wote wameshiriki.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila moja amejitajidi kujituma mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.

Tunazihitaji alama tatu za kesho ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo na kuwafurahisha mashabiki wetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER