Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Coastal Union.
Wachezaji wote wamefanya mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho ambao ni wakutafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja yupo tayari kuipambania timu kama atapata nafasi ya kucheza.
Kocha Fadlu Davids ameweka wazi kuwa tunaupa umuhimu mkubwa na tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa lengo la kutafuta ushindi.