Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Ijumaa nchini Ivory Coast.

Wachezaji wote wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo na hakuna ambaye amepata majeraha yoyote.

Baada ya mazoezi hayo usiku wa kuamkia kesho kikosi kitaanza safari ya kuelekea nchini Ivory Coast tayari kwa mchezo huo.

Tumeupa umuhimu mkubwa mchezo huo kwakuwa tunaamini tukipata matokeo chanya tutakuwa tumejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga kwenye hatua ya robo fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER