Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya kesho kuanza safari ya kuelekea Visiwani Zanzibar tayari kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Kikosi kilirejea mazoezini Disemba 27 baada ya mapumziko ya sikukuu ya Krismasi na sasa kipo tayari kwa michuano hiyo.

Wachezaji wote isipokuwa walioitwa timu za Taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON tunatarajia kusafiri nao kwa ajili ya michuano hiyo ambayo tumepangwa kundi B pamoja na timu za JKU, Singida Fountain Gate na APR ya Rwanda.

Mchezo wetu wa kwanza wa michuano hiyo utakuwa Januari Mosi ambapo tutacheza dhidi ya JKU saa 2:15 usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER