Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni.

Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Kagera ni moja ya timu ambayo huwa inatusumbua kila tunapokutana nayo lakini tumejipanga kuhakikisha tunawadhibiti na ili kupata ushindi.

Tunajua haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa wapinzani lakini tupo tayari kuhakikisha tunapata ushindi na kubaki na alama tatu nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER