Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mkwakwani

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa saa 12 jioni.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna ambaye amepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Tunauchukulia mchezo wa kesho kwa umuhimu mkubwa na lengo letu ni kuhakikisha tunashinda na kuchukua pointi zote tatu.

Coastal ni timu bora na ipo kwenye kiwango kizuri kwa sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER