Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mkwakwani

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mkwakwani tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa saa 10 jioni.

Wachezaji wote 22 ambao tumesafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho.

Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Coastal lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuondoka na alama zote tatu.

Kwa sasa kila mchezo kwetu ni fainali hatupo tayari kupoteza alama kwakuwa lengo letu ni kurejesha taji letu la ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER