Timu yafanya mazoezi ya mwisho Misri

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano wa African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly.

Kikosi kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Cairo International ambao tutautumia katika mchezo wa kesho.

Wachezaji wote 24 ambao tumesafiri nao wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo na hakuna aliyepata changamoto yoyote ambayo itamfanya kuukosa mchezo.

Hali ya hewa haitofautiani na jijini Dar es Salaam ni joto ambalo wachezaji wamelizoea hivyo hakutakuwa na changamoto yoyote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER