Timu yafanya mazoezi ya mwisho Liti

KIkosi chetu kimefanya mazoezi mwisho katika Uwanja wa Liti hapa Singida tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa saa 10 jioni.

Wachezaji wote tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya asiwe sehemu ya kikosi.

Kila mchezaji ameonyesha jitihada kubwa mazoezini na morali zao zipo hivyo matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa.

Tunajua itakuwa mechi ngumu, tunaiheshimu Ihefu kutokana nakuwa na kikosi imara lakini tumejipanga kuwakabili lengo likiwa kuchukua pointi zote tatu.

Alama tatu katika mchezo wa kesho ni muhimu sana kwetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER