Timu yafanya mazoezi ya mwisho Levy Mwanawasa

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Levy Mwanawasa tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos.

Kwa mujibu wa kanuni ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) timu mgeni anatakiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi ili kuzoea hali ya uwanja.

Wachezaji wote 24 ambao tumesafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu yoyote ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa kuwaheshimu Power Dynamos lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER