Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma kujiandaa na mchezo Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kesho saa 10 jioni.
Wachezaji wote 25 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hasa ukizingatia wapo nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi zote tatu.