Timu yafanya Mazoezi ya mwisho kwa Mkapa

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya utakaopigwa saa moja usiku.

Wachezaji wawili, Mohamed Ouattara na Augustine Okrah ambao ni majeruhi ndio pekee ambao hawakushiriki mazoezi hayo kutokana nakuwa majeruhi lakini wengine wote wameshiriki.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejaribu kuonyesha jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kuanza kesho.

Mchezo wa kesho ni kama fainali kwetu tunahitaji kupata pointi tatu ili tufuzu hatua ya robo fainali ndio maana tutapigana kufa na kupona ili kushinda.

Pamoja na maandalizi tuliyofanya na ubora tulionao pia tupo nyumbani lakini tunawaheshimu Horoya na hatutaki kufanya kosa lolote litakalotufanya tukose pointi tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER