Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tayari kwa mchezo wa kesho wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli utakaopigwa kesho saa 10 jioni.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo hayo na wameonekana morali ipo juu na wapo tayari kuipambania timu ili kutinga hatua ya makundi.
Kila mchezaji amejitahidi kuonyesha uwezo wake ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kucheza mchezo wa kesho.
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini tutaingia tukiwa na lengo moja la kuhakikisha tunafuzu hatua ya makundi.