Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Singida Kesho

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa kesho katika dimba la Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata majeraha yoyote ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa kesho.

Benchi la ufundi limeendelea kuwasisitiza wachezaji umuhimu wa ushindi katika mchezo wa kesho kwakuwa tunaelekea katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tunafahamu Singida ni miongoni mwa timu zilizosajili vizuri msimu huu na ina benchi bora la ufundi lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda hasa tukiwa katika Uwanja wa nyumbani.

Ushindi kwenye mechi ya kesho itatuongezea morali kuelekea mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ya Guinea utakaopigwa ugenini Februari 12.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER