Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC.
Mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku tunategemea utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu.
Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wamejitahidi kuonyesha uwezo mkubwa ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi ya kucheza kesho.
Tunaiheshimu Ihefu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda ili kuendelea kubaki katika nafasi za juu kwenye msimamo.