Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na CSKA

 

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Alawir kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow utakaopigwa kesho saa tisa alasiri kwa saa za nyumbani.

Kama ulivyokuwa mchezo wa jana dhidi ya Al Dhafrah mechi ya kesho pia itapigwa katika Mji wa Abu Dhabi hivyo kikosi kitaondoka Dubai mchana.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anaridhishwa na jinsi wachezaji wanavyopokea mafunzo yake ambapo ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kikosi kitakaporejea Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER