Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Coastal

 

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wa kesho wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha timu inapata matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo.

Hata hivyo tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukifahamu utakuwa mgumu na tunawaheshimu Coastal lakini lengo letu ni ushindi pekee.

Taji la ASFC ni moja ya malengo tuliyojiwekea msimu huu hivyo kila mchezo kwetu ni fainali mpaka tutakapo fanikiwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER