Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na APR

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kuikabili APR ya Rwanda katika mchezo watatu wa michuano ya Kombe Mapinduzi.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Morali za wachezaji zipo juu na tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na lengo la kuibuka na ushindi ili kumaliza hatua ya makundi bila kudondosha pointi.

Mchezo wetu dhidi ya APR utapigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER