Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Al Dhafrah

 

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika Uwanja wa Alawir kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Dhafrah utakaopigwa kesho saa 10 jioni kwa saa za Tanzania.

Kikosi kitaondoka kesho kuelekea Abu Dhabi ambako mchezo huo utafanyika na wachezaji wote wameshiriki mazoezi ya mwisho.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahishwa na jinsi wachezaji wanavyojituma na kushika vizuri mafunzo anayowapa.

Morali ya wachezaji ipo juu wanafanya jitihada mazoezini ili kumshawishi Kocha Robertinho awape nafasi.

Aidha, mshambuliaji Moses Phiri naye ameanza mazoezi mepesi baada ya kupona majeraha yake yaliyomfanya kukosa mechi mbili za mwisho za ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER