Timu yafanya mazoezi ya mwisho KMC Complex

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambao utapigwa kesho saa 10 Jioni katika Uwanja wa KMC Complex.o saa 10 Jioni katika Uwanja wa KMC Complex.

Mazoezi ya jioni yamefanyika katika Uwanja wa KMC Complex ambao utatumika katika mchezo wa kesho pia.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi yetu ya hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

Mchezo dhidi ya Tripoli utapigwa Septemba 15 nchini Libya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER