Timu yafanya mazoezi ya mwisho Kirumba

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba kujiandaa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigiwa saa 10 jioni.

Wachezaji wote isipokuwa Moses Phiri wamefanya mazoezi na wapo tayari kwa mchezo huo muhimu ambao pointi tatu ndiyo kitu pekee tunachohitaji.

Tutaingia katika mchezo wa kesho kwa tahadhari na kuiheshimu KMC kwa kuwa tunahitaji kupata alama tatu.

Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu na KMC wataingia uwanjani kwa kuhitaji alama tatu lakini tupo tayari kupambana na kuwakabili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER